Online Job Application Portal
MUHIMU: KWA WAOMBAJI WOTE
Sifa za Mwombaji
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 50
- Asiwe mwajiriwa wa Serikali au mwajiriwa wa Hospitali za
Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na
Serikali.
- Awe na sifa na weledi kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo
ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009.
Maombi yote yaambatishwe na nyaraka zifuatazo
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa
- Nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne/Sita na
Stashahada/Shahada kulingana na Kada iliyoainishwa
- Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje waambatishe
cheti cha Ithibati kutoka Baraza la Mitihani Tanzania
(NECTA).
- Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts). Aidha,
waliosoma vyuo vya nje ya Nchi, waambatishe cheti cha
Ithibati kutoka TCU
- Wasifu (C.V).
- Nakala ya cheti cha Usajili/Leseni hai ya taaluma husika (Full
Registration/Valid Licence).
- Picha ndogo (Passport size) moja ya hivi karibuni.
- Nakala ya Kitambulisho cha uraia (NIDA)/Namba ya
Utambulisho ya NIDA
- Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja
na Cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo
cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na
kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo
ya Makazi
Namna ya kuwasilisha maombi
- Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili (2) kuanzia
tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (Mwisho wa kutuma maombi
ni Tarehe 10/02/2023). Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo
wa ajira wa Wizara unaopatika kupitia tovuti ajira.moh.go.tz.
Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha
maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa
kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote
zinazohitajika.